Kenya National Anthem

1

Ee Mungu nguvu yetu
Ilete baraka kwetu,

Haki iwe ngao na mlinzi
Natukae na undugu,

Amani na uhuru
Raha tupate na ustawi.

2

Amkeni ndugu zetu
Tufanye sote bidii,

Nasi tujitoe kwa nguvu
Nchi yetu ya Kenya,

Tunayoipenda
Tuwe tayari kuilinda.

3

Natujenge taifa letu
Ee, ndio wajibu wetu,

Kenya istahili heshima
Tuungane mikono,

Pamoja kazini
Kila siku tuwe na shukrani.

1

O God of all creation
Bless this our land and nation,

Justice be our shield and defender
May we dwell in unity,

Peace and liberty
Plenty be found within our borders.

2

Let one and all arise
With hearts both strong and true,

Service be our earnest endeavour,
And our Homeland of Kenya,

Heritage of splendour,
Firm may we stand to defend.

3

Let all with one accord
In common bond united,

Build this our nation together
And the glory of Kenya,

The fruit of our labour
Fill every heart with thanksgiving.